Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilitangaza ajira za mkataba kwa kada za afya kupitia Mradi wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto (TMCHIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Mwezi Aprili 2023, TAMISEMI ilipata kibali cha kuajiri watumishi 8,070 wa kada mbalimbali za afya. Baadhi ya waombaji wenye sifa walibaki katika kanzi data ya TAMISEMI baada ya mchakato wa awali, na hivyo kuajiriwa kupitia mradi wa TMCHIP.
Waombaji waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hilo. Wanatakiwa kuwasilisha vyeti halisi vya elimu na usajili wa mabaraza ya kitaaluma kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua za ajira. Pia, hawataruhusiwa kubadilisha vituo vya kazi walivyopangiwa.
Kwa taarifa zaidi na kuona orodha kamili ya majina ya walioitwa kazini, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kupitia kiungo hiki