Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Stashahada Toleo la Pili 2025 Unapatikana www.moe.go.tz www.heslb.go.tz
Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi Wote Wanaomba Mikopo DIPLOMA
Waombaji wote wa mikopo ya elimu kwa ngazi ya Stashahada kwa mwaka wa masomo 2025/2026 wanafahamishwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Kusoma na kufuata taratibu za maombi katika Mwongozo wa mwaka wa masomo 2025/2026.
- Kuhakikisha kuwa namba ya mtihani wa kidato cha nne atakayoitumia mwombaji iwe sawa na aliyoombea udahili wa chuo.
- Kuhakikisha kuwa fomu ya maombi ya mkopo na mkataba zimesainiwa na viongozi wa serikali ya mtaa, mdhamini na kamishna wa viapo.
- Waombaji wajaze fomu zao kwa ukamilifu na kuzisaini kabla ya kuziwasilisha HESLB kwa njia ya mtandao.
- Kuhakikisha kwamba vyeti vya kuzaliwa/vifo vimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) au Afisa aliyeteuliwa.
- Kwa mwombaji mwenye akaunti ya benki ajaze taarifa zake kwa usahihi kwenye fomu ya maombi ya mkopo.
- Kwa mwombaji mwenye Namba ya simu na kitambulisho cha taifa (NIDA) ahakikishe anajaza namba hizo wakati wa kuomba mkopo.
- Waombaji wote wanakumbushwa kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.
Kufunguliwa Dirisha la Maombi Awamu ya Pili
Kwa wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu kwa ngazi ya Stashahada kwa awamu ya pili, dirisha la maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2025/2026 limefunguliwa kwa siku 14 kuanzia tarehe 21 Disemba, 2025 hadi tarehe 04 Januari, 2026.
Sifa Stahiki
Vigezo vya msingi vya mwombaji mkopo ni pamoja na:
- Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 27.
- Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu ya ngazi ya kati nchini.
- Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo kupitia mfumo wa OLAMS.
- Asiwe na ajira inayompatia mshahara.
- Awe amehitimu elimu kati ya mwaka 2019 hadi 2024.
Upangaji wa Mikopo
Upangaji wa mikopo utazingatia vipaumbele vya kitaifa, ufaulu wa kitaaluma, na hali ya kijamii.
Nyaraka za Kuambatisha
Pamoja na nyaraka nyingine, waombaji wanapaswa kuambatisha:
- Cheti cha kuzaliwa kutoka RITA au ZCSRA.
- Vyeti vya vifo kuthibitisha uyatima.
11.0 Ada ya Maombi ya Mkopo
Ada ya maombi ni shilingi elfu thelathini (30,000.00).
13.0 Maulizo na Malalamiko
Kwa maswali au malalamiko, waombaji wanapaswa kuwasiliana kupitia dawati la msaada la HESLB.
ifanyeje iwapo nimesahau neno langu la siri (Password)?
Jibu: Utapaswa kubofya kiunganishi cha “Forgotten the Password?” na kisha utapata neno jipya la siri hapo hapo (kwenye screen) mtandaoni.
Je, ni wapi nitahakiki cheti za kuzaliwa au kifo cha mzazi?
Jibu: Vyeti vya kuzaliwa na vya vifo vya wazazi lazima vihakikiwe na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kabla havijapakiwa (uploaded) kwenye mtandao (olams)