Jinsi ya kupata namba ya NIDA Online (Fahamu Namba ya NIDA (NIN))

Kitambulisho cha taifa (NIDA)ni nyenzo muhimu inayokuwezesha kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi, na kiusalama. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) nchini Tanzania imeanzisha mfumo wa kitaifa wa utambuzi wa watu ambao unatoa namba ya utambulisho wa taifa (NIN). Kupitia namba hii, mtu anaweza kufaidika na huduma nyingi, kuanzia usajili wa laini za simu mpaka kukata hati za kusafiria. Katika makala hii, tutakuonyesha jinsi ya kupata namba ya NIDA kupitia mtandao kwa urahisi.

Umuhimu wa Kitambulisho cha Taifa

Kitambulisho cha Taifa kinachotoa Namba ya NIDA (NIN) ni muhimu sana katika maisha ya kila siku.  Unaweza kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN)/Kitambulisho cha Taifa (NID) kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama:-

  • Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration),
  • Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN),
  • Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA,
  • Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport),
  • Kukata Leseni ya Udereva,
  • Kupata Huduma ya Afya,
  • Kufungua Akaunti ya Benki,
  • Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi za Fedha,
  • Kujiunga na Elimu Ngazi Mbalimbali,
  • Kupata Mkopo wa Elimu ya Juu,
  • Hati Miliki ya Kiwanja, Nyumba n.k,
  • Kujidhamini na Kudhamini Wengine,
  • Kitambulisho cha Taifa kutokana na kuwa na Kisilikoni (Cheap) kinaweza Kutumika kama Pochi ya Fedha ya Kielektroniki (E-Wallet) ambako unahifadhi fedha na kufanya malipo kwa kutumia Kitambulisho Chako,
  • Kitambulisho kinaweza kutumika kama ATM CARD,
  • Kwenye Maingio ya Malango Kielektroniki (E-Entrace),
  • Daftari la Mahudhurio la Kielektroniki (Electronic Attendance),
  • Mwananchi kuondokana na Adha ya Kubeba Utitiri wa Vitambulisho kwani sasa taarifa zote Muhimu za mwananchi zitapatikana katika Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu,
  • Kinaweza kutumika kama hati ya Utambuzi wa Utaifa wa wananchi wanaovuka mipaka ndani ya nchi zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko,
  • Vitaimarisha Utendaji Kazi Serikalini kwa Kuwa na Kumbukumbu Sahihi za Watumishi na Malipo ya Stahili zao, hasa Wanapostahafu,
  • Kupata Ruzuku za Pembejeo za Kilimo Kirahisi,
  • Kujisajili kwenye Chama cha Ushirika (Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Makundi mengine),
  • Kupata Msaada wa TASAF unaotolewa kwa Kaya Masikini,
  • Kufungua Akaunti ya Benki,
  • Kuomba Ajira pamoja na Huduma Nyingine Nyingi.

Kwa hivyo, namba yako ya NIDA inasaidia kuhakikisha kuwa unapata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazohusiana na maisha yako ya kila siku kwa uharaka na urahisi zaidi.

1Namna ya Kuangalia Namba yako ya NIDA (NIN)

Ili kufahamu namba yako ya NIDA kwa urahisi, fuata hatua hizi za mchakato:

  1. Tembelea Tovuti ya NIDA: Nenda kwenye portal rasmi ya NIDA ONLINE PORTAL SERVICES kupitia linki https://services.nida.go.tz/ kwa huduma mbalimbali za mtandaoni.
  2. Chagua ‘ Self Service (Jihudumie NIDA- Mwananchi)’: Katika tovuti, utaona sehemu ya huduma mbalimbali. Pata chaguo la Namba ya malipo na Kupata NIN.
  3. Chagua kipengele cha Fahamu Namba ya NIDA (NIN) na Jaza Fomu ya Maombi: Utahitajika kujaza taarifa zako kwa usahihi kama ifuatavyo:
  1. Jina la Kwanza (Firstname)
  2. Jina la Mwisho (Surname)
  3. Tarehe ya Kuzaliwa (DD-MM-YYYY)
  4. Jina la Kwanza la Mama
  5. Jina la Mwisho la Mama
  6. Ingiza Neno la Usalama: Baada ya kujaza taarifa hizo, ingiza neno la usalama lililoonyeshwa kwenye fomu.
  7. Tuma Ombi: Baada ya kukamilisha yote, tuma ombi lako. Utaweza kupata taarifa kuhusu namba yako ya NIDA mara baada ya mchakato kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top