Matokeo ya kidato cha sita 2025 mkoa wa Dodoma/Necta form six results 2025 Dodoma

Matokeo ya kidato cha sita 2025 mkoa wa Dodoma/Necta form six results 2025 Dodoma

Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) ni muhimu sana kwa wanafunzi wanaotarajia kujiendeleza katika elimu ya juu baada ya kufanya mtihani huu. Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (au Matokeo ya Form Six 2024) ni moja ya vigezo vinavyotumiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) katika kuwachagua wanafunzi wa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kwa hivyo, maelfu ya wanafunzi ambao ndoto zao ni kuendelea na masomo ya elimu ya juu wanayasubiri matokeo haya kwa hamu kubwa.

Ikiwa wewe ni mwanafunzi unayetaka kuangalia matokeo yako au mzazi anayetaka kujua matokeo ya mtoto wako mara tu yanapotangazwa na NECTA, fuatilia ukurasa huu kwa karibu. Katika makala hii, tumetoa maelekezo ya hatua kwa hatua juu ya jinsi ya kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita mara yatakapotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Muhtasari wa Matokeo ya Kidato cha Sita 2024/2025 – ACSEE Results

Matokeo ya ACSEE 2024/2025 ni matokeo ya mtihani wa mwisho wa Kidato cha Sita uliyoendeshwa mwezi Mei, kuanzia tarehe 6/05/2024 hadi 24/05/2024. Lengo la mtihani huu lilikuwa ni kutathmini uelewa, maarifa, na uwezo wa wanafunzi kuendelea na elimu ya juu kama vile stashahada na shahada.

Mtihani wa Kidato cha Sita 2024 (ACSEE) na Matokeo Yake

Mtihani wa Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) 2024 ulijumuisha masomo mbalimbali ambayo wanafunzi walifanyiwa tathmini, yakiwa yamegawanyika katika mchepuo wa Sayansi na Sanaa.

Michepuo ya Sayansi ni pamoja na:

•Fizikia, Kemia, na Hisabati (PCM)

•Fizikia, Kemia, na Biolojia (PCB)

•Fizikia, Jiografia, na Hisabati (PGM)

•Uchumi, Jiografia, na Hisabati (EGM)

•Kemia, Biolojia, na Jiografia (CBG)

•Kemia, Biolojia, na Kilimo (CBA)

•Kemia, Biolojia, na Lishe ya Binadamu (CBN)

Michepuo ya Sanaa ni pamoja na:

•Historia, Jiografia, na Lugha ya Kiingereza (HGL)

•Historia, Jiografia, na Kiswahili (HGK)

•Historia, Kiswahili, na Lugha ya Kiingereza (HKL)

•Kiswahili, Lugha ya Kiingereza, na Kifaransa (KLF)

•Uchumi, Biashara, na Uhasibu (ECA)

•Historia, Jiografia, na Uchumi (HGE)

Matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita huamua kozi ambayo mwanafunzi atachukua katika elimu ya juu. Baadhi ya kozi zinahitaji alama za juu ili mwanafunzi aweze kudahiliwa, kwa mfano, mwanafunzi anayelenga kusomea udaktari lazima awe na ufaulu mzuri katika mchepuo wa PCB (Fizikia, Kemia, na Biolojia).

Tarehe ya Kutangazwa kwa Matokeo ya ACSEE 2024

Kwa kuzingatia mwenendo wa miaka ya nyuma, NECTA hutangaza matokeo ya Kidato cha Sita ndani ya wiki mbili za kwanza za mwezi Julai. Kwa hivyo, mwaka huu inatarajiwa kuwa Baraza la Mitihani la Taifa litatoa matokeo haya ndani ya muda huo.

Wanafunzi wote wanashauriwa kufuatilia tovuti rasmi ya NECTA (www.necta.go.tz) au ukurasa huu kwa taarifa rasmi kuhusu matokeo haya.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2024 (ACSEE Results)

Kupitia Tovuti ya NECTA

1.Tembelea tovuti ya NECTA:https://necta.go.tz/

2.Nenda kwenye sehemu ya “Results”.

3.Chagua “ACSEE Results”.

4.Fungua ukurasa wa “ACSEE Results 2024” ili kuona matokeo ya mwaka 2024.

5.Tafuta jina la shule yako kwenye orodha iliyopo.

6.Bofya jina la shule yako ili kuona matokeo yake.

7.Baada ya kufungua matokeo ya shule yako, tafuta jina lako ili kuona matokeo yako binafsi.

Kupitia USSD Code kwa Simu ya Mkononi

1.Piga namba 15200#

2.Chagua namba 8: ELIMU

3.Chagua namba 2: NECTA

4.Chagua huduma ya 1: MATOKEO

5.Chagua aina ya mtihani: 2: ACSEE

6.Ingiza namba yako ya mtihani na mwaka mfano: S0334-0556-2024

7.Chagua aina ya malipo (Gharama ya SMS ni Tsh 100/=)

8.Baada ya malipo, utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo yako.

Kupakua Matokeo ya Kidato cha Sita 2024/2025 – PDF

Wanafunzi wanaweza kupakua matokeo yao kwa muundo wa PDF kupitia tovuti ya NECTA mara tu yatakapotangazwa rasmi.

Fursa za Elimu kwa Wanafunzi Waliofaulu Kidato cha Sita

Baada ya kufaulu mtihani wa Kidato cha Sita, wanafunzi wanaweza kuendelea na elimu ya juu katika ngazi ya stashahada (diploma) au shahada (degree).

Hatua Muhimu za Kuchukua kwa Waliofaulu Kidato cha Sita

•Tafiti vyuo na kozi unayotaka kusoma kwa kupitia kitabu cha mwongozo wa udahili wa TCU 2024/2025.

•Jiandae kuomba mikopo ya elimu ya juu kupitia HESLB, hakikisha umeandaa nyaraka zote muhimu kwa ajili ya maombi.

•Andaa ada za maombi ya chuo, inashauriwa kutuma maombi katika vyuo zaidi ya kimoja ili kuongeza nafasi ya kuchaguliwa.

Kwa Wale Ambao Hawakufanya Vizuri Sana

•Wanaweza kuomba nafasi katika vyuo vya stashahada (diploma), kwani ushindani wa kuingia kwenye diploma ni mdogo ukilinganisha na shahada.

•Wale waliopata alama za wastani wanashauriwa kuepuka vyuo vikuu vya serikali vyenye ushindani mkubwa na badala yake waombe katika vyuo binafsi ili kuongeza nafasi zao za kuchaguliwa.

Kwa maelezo zaidi, endelea kufuatilia tovuti ya NECTA au mitandao ya kijamii ya baraza kwa habari rasmi kuhusu Matokeo ya Kidato cha Sita 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top