Wizara ya Afya imetangaza nafasi 231 za ajira mpya kwa Watanzania wenye sifa stahiki. Nafasi hizi zinajumuisha kada mbalimbali kama vile Daktari Bingwa, Afisa Fiziotherapia, na Mhandisi wa Biomedical.
Sifa za Waombaji:
•Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa wale walioko kazini serikalini.
•Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu walionao.
•Kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
•Kuwasilisha wasifu binafsi (CV) yenye taarifa za mawasiliano na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
•Kuambatisha vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ikijumuisha vyeti vya kidato cha nne, sita, na vya kitaaluma kulingana na nafasi inayotakiwa.
Jinsi ya Kutuma Maombi:
Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira Portal:
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19 Machi, 2025.
Kwa maelezo zaidi na orodha kamili ya nafasi zinazopatikana, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya Wizara ya Afya:
Hakikisha unakamilisha maombi yako kwa usahihi na kuambatisha nyaraka zote muhimu kabla ya tarehe ya mwisho iliyotajwa.