Nafasi za Kazi Polisi Tanzania Machi 2025

Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya kidato cha nne, kidato cha sita, astashahada, stashahada, na shahada.

Sifa za Waombaji:

•Uraia: Raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, wazazi wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

•Umri:

•Kidato cha nne, sita, na astashahada: Miaka 18 hadi 25.

•Stashahada na shahada: Miaka 18 hadi 30.

•Urefu:

•Wanaume: Angalau futi 5 na inchi 8.

•Wanawake: Angalau futi 5 na inchi 4.

•Afya: Afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa serikali.

•Nyinginezo:

•Uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha.

•Kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA.

•Kuwa tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi na kufanya kazi mahali popote Tanzania.

•Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo) wala kumbukumbu za uhalifu.

Maombi:

Waombaji wanatakiwa kuandika barua za maombi kwa mkono, wakitumia anuani ya:

Mkuu wa Jeshi la Polisi, S.L.P 961, Dodoma.

Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi katika mfumo wa ‘pdf’.

Maombi yote yafanyike kupitia mfumo wa Ajira wa Polisi unaopatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi:

TUMA MAOMBI HAPA

Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe, au kwa mkono hayatapokelewa.

Mwisho wa Kupokea Maombi: Aprili 4, 2025.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi Tanzania:

Pia, unaweza kutazama tangazo rasmi la ajira mpya za Jeshi la Polisi Tanzania 2025 kupitia video ifuatayo:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top