Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ametoa tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa waombaji waliotuma maombi ya kazi mbalimbali. Usaili huu unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 26 Aprili 2025. Nafasi zinazohusika ni pamoja na:
•Mwalimu Daraja la III A
•Mwalimu Daraja la III B
•Mwalimu Daraja la III C
•Mwandishi Mwendesha Ofisi II
•Mlezi wa Watoto
•Mhudumu wa Usafi
Usaili utahusisha sehemu tatu: usaili wa kuandika (written), usaili wa vitendo (practical), na usaili wa ana kwa ana (oral). Waombaji wote wanatakiwa kufika na vyeti halisi vyao pamoja na kitambulisho cha utambulisho. Pia, kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri, na malazi.
Kwa maelezo zaidi na orodha kamili ya majina ya walioitwa kwenye usaili, tafadhali tembelea tangazo rasmi kupitia kiungo hiki: Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili – Halmashauri ya Jiji la Mbeya.