Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoajiametangaza kuwa Usaili vijana waliomba ajira ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia mfumo wa ajira ZIMAMOTO RECRUITMENT (ajira.zimamoto.go.tz) utafanyika kuanzia tarehe 05 hadi tarehe 17 Aprili, 2025 kuanzia saa 1:00 asubuhi kwa kila kundi.
Sehemu ya Usaili Kwa wenye elimu ya kidato cha nne
Kwa waombaji waliomba ajira hizi kwa elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 09 Aprili, 2025 saa 1:00 asubuhi kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.
Sehemu ya Usaili Kwa Waombaji wenye elimu ya Shahada na taaluma mbalimbali.
Waombaji wenye elimu ya Shahada na taaluma mbalimbali usaili wao utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma kuanzia tarehe 14 Aprili hadi 17 Aprili, 2025, saa 1:00 asubuhi kwa kila kundi.