Chuo Kikuu cha College of African Wildlife Management (CAWM), kilichopo Mweka, Kilimanjaro, ni taasisi inayotambulika kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori. Chuo hiki, kilichoanzishwa mwaka 1963, kimekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya uhifadhi nchini Tanzania na kimataifa.
Sifa za Kujiunga na Chuo Kikuu Cha College of African Wildlife Management ni vigezo vinavyohitajika ili kuthibitisha uwezo na sifa za waombaji wa programu mbalimbali zinazotolewa. Hizi ni muhimu kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaoingia wanakidhi viwango vya kitaaluma vya taasisi.
Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Shahada ya Kwanza katika CAWM
Kwa waombaji wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu Cha CAWM, wanatakiwa kuwa na angalau alama mbili za daraja kuu katika masomo ya Biolojia, Kemia, Fizikia, Jiografia, Lugha ya Kingereza, Kilimo, Sayansi ya Kompyuta, Lishe, au Hisabati ya Juu. Chuo kinatoa shahada mbalimbali ikiwemo katika Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii.
Sifa na Vigezo vya Jumla kwa Kwa waombaji wa kidato cha sita (General Minimum Entry Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kabla ya 2014 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
2 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita mnamo 2014 na 2015 | Passi mbili kuu (‘C’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 kutoka kwa masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1; E = 0.5) |
3 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kuanzia 2016 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
Sifa na Vigezo vya Jumla Kwa waombaji wa Diploma (For Holders of Ordinary Diploma or Equivalent Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waombaji wa Stashahada ya Kawaida, FTC na Sawa | Angalau pasi nne (“D” na zaidi) katika “O” Level au NVA Level III na chini ya pasi nne “O” Level au sawa na sifa za kigeni kama ilivyothibitishwa na NECTA au NACTVET; na i) Angalau GPA ya 3.0 kwa Stashahada ya Kawaida (NTA Level 6); au ii) Wastani wa alama “C” kwa Cheti cha Fundi Kamili (FTC) (ambapo A=5, B=4, C=3, na D=2); au iii) Wastani wa alama “B” kwa Stashahada ya Elimu ya Ualimu; au iv) Wastani wa alama “B” kwa tuzo zinazohusiana na Afya kama Tiba ya Kliniki na nyinginezo; au v) Alama ya Heshima kwa Stashahada na vyeti visivyofungamana na NTA; au vi) Upper Second Class kwa stashahada zisizo za NTA. |
2 | Cheti cha Msingi cha OUT | GPA ya 3.0 iliyokusanywa kutokana na masomo sita muhimu na angalau Alama ya “C” kutoka masomo matatu katika klusta husika (Sanaa, Sayansi na Masomo ya Biashara) pamoja na Cheti cha Juu cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari kilicho na alama angalau 1.5 kutoka masomo mawili; au Stashahada ya Kawaida kutoka taasisi inayotambuliwa yenye GPA ya angalau 2.0 AU NTA level 5 / Cheti cha Fundi wa Kitaalam Kiwango cha II. |
Ili kupata orodha kamili ya programu na sifa za kujiunga na Chuo Kikuu Cha CAWM, waombaji wanashauriwa kupakua Mwongozo wa TCU kupitia linki TCU Guidebooks.