Tarehe 7 Machi 2025, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, ilitoa tangazo la kuitwa kazini kwa waombaji waliofaulu usaili katika nafasi mbalimbali, ikiwemo walimu na kada nyingine. Waombaji waliofaulu wanapaswa kuchukua barua za kupangiwa vituo vya kazi katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya tangazo. Baada ya muda huo, barua ambazo hazitachukuliwa zitatumwa kupitia anuani za posta za wahusika.
Majina ya waombaji waliofaulu na maelezo zaidi yanapatikana kwenye tangazo hilo. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo, wanashauriwa kuendelea kuomba nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
TAZAMA MAJINA HAPA