Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi Uhamiaji 2025

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anatangaza kwa Vijana walioteuliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kufika katika Chuo cha Uhamiaji Raphael Kubaga kilichopo Boma Kichakamiba, Wilaya ya Mkinga – Mkoa wa Tanga, siku ya Jumamosi tarehe 1 Machi 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.

Wale watakaofika chuoni baada ya muda tajwa hawatakubaliwa. Kwa wale waliotuma maombi na kuteuliwa kupitia Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, wanapaswa kuripoti katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja (Tunguu) siku ya Jumatatu tarehe 24 Februari 2025 saa 2:00 asubuhi.

NYARAKA AMBAZO MWANAFUNZI ANAPASWA KUPELEKA CHUONI

Mwanafunzi anapaswa kuripoti akiwa na vyeti halisi vya elimu na taaluma mbalimbali. Mwanafunzi ambaye hatakuwa na nyaraka halisi hatakubaliwa chuoni. Vyeti na nyaraka zinazohitajika ni kama ifuatavyo:

1.Cheti cha kuzaliwa

2.Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA

3.Vyeti halisi vya Elimu vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita na Shahada

4.Vyeti vya Ujuzi mbalimbali (Kwa wenye ujuzi)

MAHITAJI MUHIMU

1.Fedha kiasi cha Tshs. 50,400/= kwa ajili ya Bima ya Afya kwa wale wasio na kadi ya Bima ya Afya au wenye kadi ya Bima ya Afya inayokwisha muda wake kabla ya tarehe 31/12/2025.

2.Fedha taslimu kiasi cha Tshs. 25,000/= kwa ajili ya vipimo vya afya.

3.Fedha za matumizi binafsi kwa ajili ya mahitaji ya kila siku.

4.Mavazi na vifaa vya binafsi:

•Seti mbili (02) za ‘truck suit’ rangi nyeusi na bluu ya giza.

•Jozi mbili (02) za viatu vya michezo (sport rubbers) za rangi yoyote.

•Seti tatu (03) za mavazi safi ya kiraia.

•Mashuka manne (04) ya rangi ya bluu.

•Mto wa kulalia mmoja (01).

•Mifuko miwili ya mto (pillowcase) ya rangi ya bluu.

•Chandalua (01) ya rangi ya bluu.

5.Vifaa vya kujifunzia:

•Daftari kubwa nne (04) za 4QRs.

6.Vifaa vya matumizi ya binafsi na usafi:

•Sanduku la chuma (trunker).

•Ndoo mbili (02) za plastiki (moja ya lita 10 na nyingine ya lita 20).

•Fulana mbili (02) za rangi ya bluu giza zenye shingo ya duara.

•Jozi moja (01) ya buti za mvua (rain boots).

•Taulo moja (01).

7.Vifaa vya usafi wa mazingira:

•Jozi moja (01) ya koleo kwa ajili ya usafi.

•Sehemu ya vifaa vya usafi ikiwa ni pamoja na:

•Spedi (01) na mpini wake.

•Slash (01).

•Panga (01).

•Reki (01).

TAARIFA MUHIMU

Vifaa vilivyotajwa vinapatikana katika Duka la Chuo, hivyo mwanafunzi anaweza kuvinunua kwa hiari yake.

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA UHAMIAJI 2025

TANGAZO:

•Gharama za usafiri kutoka nyumbani hadi Chuoni zitagharamiwa na mwanafunzi mwenyewe.

•Wale walioteuliwa kujiunga na mafunzo watafanyiwa uchunguzi wa afya kabla ya kuanza mafunzo, na wote watakaobainika kuwa na changamoto za kiafya hawataruhusiwa kujiunga na Chuo kwa ajili ya mafunzo.

•Orodha ya majina ya walioitwa kwenye mafunzo inapatikana kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji (www.immigration.go.tz).

>> PAKUA ORODHA YA WALIOCHAGULIWA HAPA <<

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top