Wito wa Usaili katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)

  1. Wito wa Usaili katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) anapenda kuwajulisha waombaji wote wa nafasi mbalimbali za ajira kuwa usaili umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 22 Februari, 2025 (usaili wa maandishi) hadi tarehe 23 Februari, 2025 (usaili wa mdomo).

📍 Mahali: Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)

🕖 Muda: Kuanzia saa 1:00 asubuhi

Waombaji wote wanahimizwa kufika kwa wakati na kuzingatia maelekezo yaliyotolewa.

Maelekezo kwa Waombaji Walioitwa Kwenye Usaili

Waombaji waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

1️⃣ Usaili utafanyika katika tarehe, muda, na eneo lililotajwa katika tangazo hili.

2️⃣ Kila mgombea anapaswa kuleta kitambulisho kwa ajili ya uthibitisho. Vitambulisho vinavyokubalika ni:

•Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

•Kitambulisho cha Mpiga Kura

•Pasipoti

•Leseni ya Udereva

•Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa/kijiji

3️⃣ Kila mgombea lazima alete vyeti halisi vya taaluma, ikiwemo:

•Cheti cha Kuzaliwa

•Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)

•Cheti cha Kidato cha Sita (Form VI)

•Cheti cha Diploma, Advanced Diploma, au Shahada kulingana na sifa za mwombaji

4️⃣ Hati za matokeo ya muda (Testimonials, Provisional Results, Statement of Results) na result slips za Form IV & VI HAZITAKUBALIWA na mgombea hataruhusiwa kushiriki usaili.

5️⃣ Gharama za chakula, usafiri, na malazi zitabebwa na mgombea mwenyewe.

6️⃣ Kila mgombea lazima afuate tarehe, muda, na eneo la usaili kwa ukamilifu.

7️⃣ Waombaji waliohitimu nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika kama vile TCU, NACTE, au NECTA.

8️⃣ Waombaji ambao majina yao hayajaonekana katika tangazo hili wanapaswa kuelewa kuwa hawakukidhi vigezo vilivyohitajika. Hata hivyo, wanahimizwa kuomba tena nafasi zitakapotangazwa upya.

9️⃣ Kwa taaluma zinazohitaji usajili katika bodi za kitaaluma, waombaji wanapaswa kuwasilisha vyeti vyao halisi vya usajili.

📄 SOMA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI KUPITIA PDF ILIYOPO HAPA CHINI:

🔗 [PAKUA HAPA PDF]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top